Harakati ya Linda Mwananchi itazuru Kaunti ya Kakamega wikendi hii inapoongeza uhamasishaji wa wananchi na kujitahidi kuimarisha uungwaji mkono kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2027. Viongozi wakiongozwa na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna wanatarajiwa kufanya mikutano katika maeneo bunge ya Butere, Shinyalu, na Ikolomani. Ziara hiyo ya siku mbili inakuja siku moja baada ya harakati hiyo kufanya mikutano huko Busia inapojitahidi kujiimarisha kama nguvu kubwa ya upinzani.
EDWIN SIFUNA – BUSIA