Mkurugenzi wamashtaka ya umma amewashtaki wavulana wanne wa shule ya upili kwa madai ya kumnajisi msichana wa miaka 17 katika Kaunti ya Homa Bay. Mahakama iliambiwa kwamba kosa hilo lilidaiwa kufanywa Julai tarehe 30 katika Kaunti Ndogo ya Rangwe. Washukiwa walikana mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkuu Mary Immaculate Gwaro na waliwekwa rumande katika Kitengo cha Ulinzi wa watoto cha Homa Bay. Kesi hiyo itasikilizwa Agosti tarehe 22.