Maafisa wa ulinzi wa kibinafsi wanawake nchini wameihimiza serikali kuimarisha uwakilishi wa wanawake ndani ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usalama wa Kibinafsi na kuanzisha mifumo ya siri ya kushughulikia unyanyasaji mahali pa kazi. Wakiongozwa na Elizabeth Samba, kundi hilo pia limetoa wito wa kuajiriwa kwa usawa wa kijinsia, kuboreshwa kwa mazingira ya kazi na kutambuliwa rasmi kwa chama cha Ubora wa Wanawake katika Ulinzi kama mdau muhimu wa tasnia hiyo.

ELIZABETH SAMBA – WOMEN