Mwenyekiti wa Shirikisho la Utalii la Kenya Fred Odhiambo ametetea kanuni zilizopendekezwa za bima ya usafiri zinazowataka wageni wanaokaa Kenya kwa hadi miezi 12, kupata bima ya afya ya usafiri yenye kiwango cha chini cha takriban KSh milioni 6.5. Akiongea kwenye NTV, Odhiambo alisema sheria hizo hazitaifanya Kenya kuwa kivutio cha watalii ghali. Aliongeza kuwa kanuni hizo bado zinaboreshwa kupitia mashauriano na wadau kabla ya utekelezaji kamili.


FRED ODEK-REFINE