Wadau katika afya ya uzazi wanaihimiza serikali kuanzisha sera sawa ya ushuru kwenye bidhaa za hedhi ili kuboresha upatikanaji na bei nafuu. Ripoti ya Mtandao wa Vijana wa Afrika (NAYA) inaonyesha kwamba ingawa bidhaa za hedhi zinazotumika mara moja hazitozwi kodi, zile zinazoweza kutumika tena hutozwa kodi kama vifaa vya matibabu na kuzifanya kuwa ghali. NAYA pia inapendekeza utoaji wa motisha ili kuwasaidia wazalishaji wa ndani katika kutengeneza bidhaa za hedhi zenye bei nafuu na ubora wa juu.


FAITH MASIKA – CUP