Zaidi ya wanariadha 1,000 watakutana Eldoret Jumapili hii, kwa ajili ya toleo la nne la mbio za Betika Uasin Gishu Half Marathon, huku bingwa mtetezi Robert Kiprop akiongoza timu imara katika kutafuta ushindi mwingine. Macho yote yatakuwa kwa mshindi huyo wa fainali za kitaifa za BingwaFest za mbio za mita 10,000, ambaye anarudi kutetea taji aliloshinda mwaka jana. Mbio za wanawake pia zinatarajiwa kutoa ushindani wa kusisimua huku mshindi mpya akitarajiwa kutawazwa wakati bingwa mtetezi Gladys Chepkurui hayupo.
Mshambuliaji wa RB Leipzig, Yan Diomande, anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake kwenda Real Madrid. Kijana huyo wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 19 aliondoka hotelini kwake Austria kukamilisha uhamisho wake kwenda Bernabue baada ya mazungumzo marefu kwa wiki tatu zilizopita. Kuna makubaliano kamili kati ya vilabu kwa uhamisho wenye thamani ya hadi pauni milioni 120 kama jumla ya kifurushi. Madrid inalipa ada ya uhakika ya pauni milioni 107 kwa raia huyo wa Ivory Coast. Pia kuna nyongeza zinazoweza kufikiwa zilizojumuishwa katika mpango huo, ambazo zinaweza kufikisha takriban pauni milioni 116.
Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Marsabit, Samburu a Moyale.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.