Mwanafunzi wa miaka 18 amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mwanafunzi mwenzake, wa miaka 9 katika choo cha shule. Katika ushahidi wake, mtoto huyo mdogo aliiambia mahakama ya Lamu kwamba siku hiyo alienda chooni wakati mshtakiwa, ambaye pia alikuwa mwanafunzi katika shule hiyo, alimfuata na kumwamuru avue nguo. Mtoto huyo mdogo aliposita, alimpiga kofi mgongoni, akimlazimisha kuvua nguo. Wanafunzi wengine wawili waliingia chooni na kuona kilichokuwa kikiendelea.