Mgombea urais wa Chama cha United Green Movement, David Maraga, leo anaendelea na ziara yake ya siku tatu ya kampeni katika Kaunti ya Taita Taveta. Ratiba ya Maraga inajumuisha mikutano na wazee, vijana na wataalamu huko Voi kabla ya kuelekea Mwatate leo kwa mazungumzo na viongozi wa mashinani na wajumbe. Ziara hiyo ni sehemu ya juhudi zake za kutangaza azma yake ya urais kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2027.