Tume ya Maadili EACC imetuma faili 43 za uchunguzi kwa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma kati ya Aprili mosi na Juni tarehe 30 mwaka huu. Kati ya faili 38 zilizopendekezwa kwa ajili ya mashtaka, nne ziliidhinishwa huku nne zikikataliwa, huku zingine zikiendelea kukaguliwa. EACC inasema hakuna kesi iliyopendekezwa kwa ajili ya mashtaka katika kipindi hicho ambayo bado imepelekwa mahakamani.