Wakaazi wa maeneo yasiyo rasmi ya Nairobi wanaendelea kukabiliwa na athari kubwa za mafuriko, utafiti mpya wa Taasisi ya Rasilimali Duniani unaonyesha. Mkurugenzi Mtendaji wa WRI Africa Wanjira Maathai anasema wanawake, watoto, wazee na watu wenye ulemavu wanaathiriwa zaidi kutokana na upatikanaji mdogo wa taarifa, uokoaji na usaidizi. Ripoti hiyo inahimiza mamlaka kushirikisha jamii katika kupanga na kuimarisha mifumo ya tahadhari za mapema ili kupunguza hatari za maafa ya siku zijazo.
WANJIRA MAATHAI - URGE