Kenya inaweza kupunguza ukopaji wake kwa kuwekeza mikopo katika miradi ya maendeleo badala ya matumizi ya kila siku ya serikali. Mwanachumi Charles Karisa anasema kupunguza matumizi mabaya ya fedha zilizokopwa na kuongeza miradi ya Ushirikiano wa Umma na Binafsi kutapunguza utegemezi wa nchi wa deni, kwani asilimia 71 ya mapato ya serikali huenda kwenye kuhudumia deni la umma la Sh. trilioni 12.8.


CHARLES KARISA - LOAN