Watu wanne wamefariki baada ya kuzikwa wangali hai wakati wakichimba choo cha shimo katika Shule ya Msingi ya Chiche huko Borabu, Kaunti ya Nyamira. Waathiriwa walinaswa udongo ulipoanguka katika eneo la ujenzi, huku juhudi za uokoaji zikifeli. Familia za marehemu sasa zinadai uchunguzi kuhusu tukio hilo, zikimtuhumu mwanakandarasi kwa uzembe na kutaka uwajibikaji kuhusu hatua za usalama katika eneo hilo.


DECEASED FAMILIES – LAMENT