Wafanyakazi wa UHC wanatarajiwa kuandamana leo, wakidai barua rasmi za uteuzi licha ya hati zao za malipo kuonyesha kuwa wako chini ya masharti ya kudumu na pensheni. Mwenyekiti wa KUCO Peterson Wachira anasema barua za uteuzi pekee ndizo zinazoweza kuthibitisha kisheria hali yao ya ajira, akiongeza kuwa maandamano yataendelea hadi ofisi ya Baraza la Magavana na Bunge. Mgomo sasa uko katika siku yake ya 10.
PETERSON WACHIRA – STRIKE