Zinedine Zidane ametia saini mkataba wa miaka minne kama kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ufaransa, hadi Juni 2030. Anachukua nafasi ya Didier Deschamps, ambaye muda wake ulianza mwaka 2012 na kumalizika mapema mwezi huu baada ya Ufaransa kumaliza katika nafasi ya nne kwenye Kombe la Dunia. Deschamps aliiongoza Ufaransa kwenye utukufu wa Kombe la Dunia la mwaka 2018 na fainali miaka minne baadaye kabla ya kustaafu baada ya mashindano ya mwaka huu. Zizou ambaye hapo awali alikuwa kocha wa Real Madrid alikuwa mwenzake Deschamps katika timu iliyoshinda Kombe la Dunia la 1998.

 

Roberto Mancini ameteuliwa kuwa meneja wa Italia kwa mara ya pili - siku moja tu baada ya Andrea Pirlo kujiondoa kwenye kinyang'anyiro cha nafasi hiyo na mkurugenzi wa ufundi Paolo Maldini kujiuzulu. Gennaro Gattuso aliacha nafasi yake kama kocha wa Italia mwezi Aprili baada ya Azzurris kushindwa kufuzu Kombe la Dunia la tatu mfululizo. Pirlo alionekana tayari kuchukua nafasi lakini Jumatatu alijiondoa kufuatia utata kuhusu uhusiano wake na kampuni ya kamari ya Urusi. Claudio Ranieri, atachukua nafasi ya Maldini kama mkurugenzi wa ufundi.


Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Kakamega, Eldoret na Kisumu.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.