Arsenal imethibitisha kwamba William Saliba hatahitaji upasuaji wa mgongo lakini atakuwa nje kwa muda mrefu. Beki huyo wa kati alitolewa mapema katika mechi ya nusu fainali ambayo Ufaransa ilishindwa na Uhispania kutokana na jeraha la mgongo na baadaye akakosa mechi yao ya mchujo ya nafasi ya tatu dhidi ya Uingereza. Saliba alikuwa akiuguza jeraha la mgongo kabla ya Kombe la Dunia na kulikuwa na wasiwasi kwamba angekosa mashindano yote. Alianza mechi nne katika safari ya Ufaransa kuelekea nusu fainali kabla ya mgongo wake hatimaye kuwa katika hali mbaya zaidi.


Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Nairobi.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.