Kiongozi wa timu ya Linda Mwananchi na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna amekutana na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Fred Matiang’i pamoja na viongozi wengine wa Abagusii. Katika chapisho la mitandao ya kijamii, Sifuna alishiriki picha za mkutano huo, na kuzua uvumi kwamba muungano wa kisiasa unaweza kuanza kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2027.