Waziri wa Michezo Salim Mvurya ametoa wito kwa wapiga kura wa eneo la Pwani kuunga mkono azma ya Rais William Ruto ya kuwania muhula wa pili. Mvurya alisema utawala wa Kenya Kwanza umeazimia kushughulikia malalamiko ya kihistoria ya ardhi yanayoathiri eneo hilo. Aliwasihi wakaazi kukumbatia umoja, na kuepuka siasa za kikabila zenye mgawanyiko.


SALIM MVURYA - COAST