Kiongozi wa Wengi Bungeni Kimani Ichung'wah amewasihi wahadhiri wa vyuo vikuu wanaogoma kutoa nafasi ya mazungumzo na kuepuka kuchukua misimamo mikali ambayo inaweza kuchelewesha utatuzi wa mgogoro wao. Mbunge huyo wa Kikuyu pia amewasihi wahadhiri kuruhusu SRC kushughulikia wasiwasi wao huku juhudi zikiendelea kutatua mgomo unaoendelea. Wahadhiri wamekuwa kwenye mgomo kwa zaidi ya wiki mbili, wakidai ufadhili wa kutosha kwa ajili ya kukamilika kwa CBA yao ya 2027-29 na malipo ya malimbikizi ya madeni.
KIMANI ICHUNG’WAH – LECTURERS