Katibu Mkuu wa Mambo ya kigeni Korir Sing'Oei anatoa wito wa mageuzi ya sheria za kimataifa ili kushughulikia vitisho vinavyoongezeka vya usalama duniani, ukosefu wa usawa na migogoro. Akizungumza katika Trust Summit 2026 jijini Nairobi, Sing'Oei alisema mfumo wa kisheria wa kimataifa ulioanzishwa baada ya Vita vya Pili vya Dunia unakabiliwa na changamoto, kwa kiasi fulani kutokana na kutengwa kwa nchi nyingi za Kusini mwa Dunia wakati wa kuundwa kwake. Alionya kwamba mabadiliko ya hali ya hewa, mikurupuko ya magonjwa na teknolojia zinazoibuka zinahitaji ushirikiano mkubwa wa kimataifa.
KORIR SING’OEI – THREATS