Naibu Rais Kithure Kindiki anasema upatikanaji wa malazi bora karibu na taasisi za masomo ni muhimu katika kuboresha matokeo ya kujifunza kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na vyuo. Akizungumza wakati wa ukaguzi wa ujenzi unaoendelea wa hosteli katika Chuo cha Mafunzo ya Ufundi cha Muraga, eneo bunge la Maara, Kaunti ya Tharaka Nithi, Kindiki alisema serikali inatumia hazina ya nyumba kutoa malazi kwa takriban wanafunzi 180,000 kote nchini. Hosteli hiyo yenye vyumba 580 imekamilika kwa asilimia 25 na itagharimu Sh260 milioni.
KITHURE KINDIKI – HOSTELS