Kupunguza kugawanya ardhi ya kilimo ni hatua muhimu katika kulinda usalama wa chakula na lishe nchini Kenya. Mtaalamu wa lishe Henry Ngethe, anasema kuwa ongezeko la idadi ya watu linahitaji sera madhubuti zaidi ili kuhakikisha nchi inaweza kulisha watu wake. Anaongeza kuwa kuna haja ya ubunifu zaidi ili kuboresha upatikanaji wa lishe bora, licha ya maendeleo yaliyopatikana hadi sasa. Kauli yake inakuja wakati dunia ikiadhimisha Siku ya Chakula Duniani leo.

 

HENRY NGETHE- FOOD