Wanawake wameonywa dhidi ya kutumia dawa za kupunguza maumivu ili kutuliza maumivu ya tumbo wakati wa hedhi, kwani kufanya hivyo kunaweza kuwasababishia matatizo ya kiafya. Mtaalamu wa afya ya uzazi, Linda Martina, anasema dawa hizo wakati mwingine zinaweza kusababisha mabadiliko katika mfumo wa hedhi na kuongeza maumivu wakati wa hedhi zinazofuata. Pia amewahimiza wasichana kwenda katika vituo vya afya iwapo watapata maumivu makali wakati wa hedhi.


LINDA MARTIN - PAIN KILLERS