Gavana wa Mombasa Abdulswamad Nassir ameipongeza serikali ya Rais William Ruto kwa kutekeleza programu zinazolenga kuharakisha maendeleo ya kitaifa. Akizungumza mjini Mombasa jana, Nassir aliipongeza Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA) kwa kupanua upatikanaji wa huduma za afya, akisema wakaazi wengi zaidi wanaweza kunufaika na huduma za matibabu. Matamshi yake yalikuja huku kaunti hiyo ikizindua uchunguzi wa kimatibabu bila malipo kwa heshima ya Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga.
ABUDUL NASSIR-SHA