Wadau wa sekta ya uchukuzi wanatoa wito wa ushirikiano wa karibu na mamlaka ili kuimarisha usalama barabarani msimu wa sikukuu wa Disemba unapokaribia. Wanasema juhudi za pamoja na uzingatiaji mkali wa sheria za trafiki ni muhimu katika kupunguza ajali, ambazo mara nyingi huongezeka wakati wa likizo. Wadau hao pia wamewasihi SACCO za usafiri wa umma, madereva, abiria na watumiaji wengine wa barabara kuchukua jukumu la kibinafsi na kuwa waangalifu wanapotumia barabara.

VOX POP-SAFETY