Vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu vinakabiliwa na shinikizo kutokana na kushindwa kuwajibikia usalama wa wanafunzi wao. Mtaalamu wa masuala ya usalama, George Musamali, anasema kuwa baadhi ya taasisi hizo huchukua idadi kubwa ya wanafunzi lakini hukosa mifumo madhubuti ya kuwafuatilia na kuwawajibikia, ikiwemo kanuni za wazi za maadili ya wanafunzi. Anazitaka taasisi hizo kuimarisha hatua za usalama kwa wanafunzi, huku kukiwa na wasiwasi unaoongezeka kuhusu vifo visivyoelezeka vya wanafunzi katika taasisi za elimu ya juu.

GEORGE MUSAMALI - SECURITY