Timu ya taifa ya wanawake ya Malawi iliifunga Zimbabwe mabao 7-0 jana na kufuzu kwa raundi ya tatu ya michuano ya kufuzu kwa Olimpiki ya mwaka 2028, kwa ushindi wa jumla wa mabao 9-0. Dada wawili, Temwa na Tabitha Chawinga, walifunga mabao, huku Chisomo Banda, Asimenye Simwaka na Sarah Mulimbika nao wakitikisa nyavu. Malawi itakutana na Harambee Starlets katika raundi inayofuata mwezi ujao, baada ya Kenya kuichapa Seychelles mabao 22-0. Timu mbili za wanawake kutoka Afrika zitafuzu kwa michuano hiyo itakayofanyika nchini Marekani kuanzia tarehe 14 hadi 30 Julai 2028.

 

Winga wa pembeni wa Gor Mahia, Shariff Musa, anasema hawataruhusu ushindi wao wa mabao 4-2 dhidi ya Muranga Seal kuwafanya wajiamini kupita kiasi, kwani hiyo ni mechi yaa kwanza tu ya msimu. Mshambuliaji huyo wa Harambee Stars alifunga mabao mawili huku 'K'Ogalo', ikipanda hadi kileleni mwa jedwali la ligi ikiwa na pointi tatu—sawa na Tusker na Shabana—lakini ikiwa na tofauti bora ya mabao. Shariff anatarajia msimu mgumu, lakini anaamini wanaweza kutetea taji lao kwa kucheza mechi mojaa baada ya nyingine.

Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Nairobi, Narok a Kajiado.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.