Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja ameonya kwamba shule katika Jiji Kuu zinaweza kufungwa ikiwa mvua ya El Nino iliyotabiriwa itakuwa tishio kwa wanafunzi. Akiwa mbele ya kamati ya Barabara na Nyumba ya seneti, Sakaja alisema kaunti imeimarisha maandalizi ya mvua kubwa na mafuriko yanayowezekana, huku maafisa wakipitia hatua za kuwalinda wakaazi na miundombinu muhimu. Gavana huyo alisema mawasiliano yatakuwa muhimu katika kuhakikisha wakaazi katika maeneo hatari wanapokea maonyo kwa wakati unaofaa.
JOHNSON SAKAJA - PANIC