Mbunge wa Kiharu, Ndindi Nyoro, amekanusha vikali madai ya Seneta wa Nyandarua, John Methu, kwamba yeye ni "jasusi wa siri" (mole) wa Rais William Ruto. Katika mahojiano ya televisheni Jumapili, Methu alidai kuwa mbunge huyo wa Kiharu ni wakala wa siri anayefanya kazi ya kugawanya upinzani kwa niaba ya Rais. Akijibu madai hayo, Nyoro alisisitiza kuwa Methu hana uhalali wa kuwakosoa wengine ilhali yeye mwenyewe anafaidika na ukarimu wa Ruto, akidai kuwa nyumba anayoishi seneta huyo ilinunuliwa na Rais.
NDINDI NYORO - LECTURE