Waziri wa Usalama, Kipchumba Murkomen, ametangaza kuwa amani na usalama vimerejeshwa katika Kerio Valley, huku akizindua mpango mkakati wa maendeleo unaojumuisha ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilomita 550, masoko tisa ya kisasa na nyumba 3,000 za gharama nafuu katika Kaunti ya Elgeyo Marakwet. Akihutubia wakazi wa Kapyego, Marakwet Mashariki, Murkomen alisema serikali inaelekeza nguvu zake katika maendeleo ya kiuchumi ili kufungua eneo hilo, kuboresha miundombinu na kuleta fursa kwa wakazi.
KIPCHUMBA MURKOMEN - JIFICHA