Kiongozi wa Chama cha Jubilee, Fred Matiang’i, amemjibu Rais William Ruto kufuatia mashambulizi yake ya hivi karibuni dhidi ya Rais mstaafu Uhuru Kenyatta, akimtaka kuzingatia kuongoza taifa badala ya kumkosoa mtangulizi wake. Akizungumza huko Kamana, Oloitoktok, Matiang’i alisema kuwa Uhuru amestaafu siasa za ushindani na anapaswa kuruhusiwa kutekeleza majukumu yake katika Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Afrika Mashariki bila kuhusishwa katika malumbano ya kisiasa.

FRED MATIANG’I - KAZI