Naibu Rais Kithure Kindiki amethibitisha tena kujitolea kwa serikali kuharakisha maendeleo ya kitaifa kupitia uwekezaji wa kimkakati katika miundombinu, kilimo, nyumba za bei nafuu na elimu. Alisema matumizi endelevu ya umma yanasalia kuwa muhimu katika kuboresha maisha na kupanua fursa za kiuchumi. Akihutubia wakaazi wa Mukurweini katika Kaunti ya Nyeri, alitangaza juhudi mpya za kuharakisha miradi ya serikali ya kitaifa iliyokwama, akisisitiza wakaazi wanastahili maendeleo bila kujali itikadi zao za kisiasa.
KITHURE KINDIKI - MAENDELEO