Mtaalamu wa afya Nduku Kilonzo amesema jamii lazima zibaki kuwa kitovu cha juhudi za kukomesha Virusi vya HIV ifikapo mwaka 2030. Kilonzo anasema kinga madhubuti ya HIV inahitaji nchi kuratibu huduma za afya na sekta zingine, ikiwa ni pamoja na huduma za kijamii na mahakama, ili kuwafikia watu wanaozihitaji. Anawasihi wasanifu wa mageuzi duniani kuhakikisha mifumo mipya ya ufadhili na uratibu inawezesha jamii za wenyeji, kuimarisha programu za kuzuia na kusaidia serikali kuhamasisha rasilimali zinazohitajika ili kudumisha mwitikio.
NDUKU KILONZO - COMMUNITIES