AI isiyodhibitiwa inaweza kuathiri jinsi wanafunzi wanavyojifunza na kusababisha maamuzi hatari ya kiafya pale watu wanapoitumia kutambua maradhi au kujipangia dawa. Mbunge wa Kikuyu, Kimani Ichung’wah, anataka serikali iingilie kati na kusimamia matumizi ya AI katika shule, vyuo vikuu na hospitali. Akizungumza Bungeni, Ichung’wah aliwataka wabunge kushirikiana na wizara za Afya na Elimu kuweka kanuni zinazolinda afya ya umma na uadilifu wa kitaaluma.
KIMANI ICHUNG’WAH - AI