Wazazi wameshauriwa kuhakikisha kuwa watoto wanatumia majukwaa ya kidijitali kwa uwajibikaji wakati wa likizo za shule. Mtaalamu wa haki za binadamu, Patricia Njeri, anasema kuwa mitandao ya kijamii na programu za mtandaoni hutoa fursa za kielimu na za kuwawezesha watoto iwapo zitatumiwa ipasavyo. Vilevile, Njeri anawataka wazazi kubeba jukumu la matendo ya watoto wao na kuwafuatilia kwa karibu, akisisitiza kuwa mwongozo sahihi ni muhimu katika kulea watu wenye uwajibikaji wanaochangia vyema katika jamii.


PATRICIA NJERI - PHONES