Wapelelezi wanachunguza kifo cha mtoto wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja, aliyefariki baada ya kudaiwa kutumbukia kwenye kisima kilichokuwa wazi katika kituo cha daycare eneo la Upepo, Kisumu Mashariki. Kwa mujibu wa polisi, mtoto huyo alikutwa akielea ndani ya kisima hicho jioni ya Jumapili. Babake aliwaeleza polisi kuwa alimpeleka binti yake katika kituo hicho kinachoendeshwa na mwanamke mmoja asubuhi. Hata hivyo, aliporejea kumchukua majira ya saa kumi na moja jioni, aliarifiwa kuwa mtoto huyo alikuwa ametumbukia kwenye kisima.