Gavana wa Kirinyaga, Anne Waiguru, anatoa onyo kwamba eneo la Mlima Kenya linaweza kusalia nje ya uongozi wa ngazi ya juu wa taifa kwa miaka mingi iwapo viongozi wake watashindwa kufanya maamuzi ya kimkakati ya kisiasa. Aliwahimiza viongozi wa eneo hilo kutathmini upya mkakati wao wa kisiasa, huku akionya dhidi ya kutegemea muungano wa upinzani. Alihoji uwezo wa upinzani wa kutoa upinzani mkali dhidi ya Rais William Ruto katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027, akitaja kuwepo kwa migawanyiko na ushindani.
ANNE WAIGURU - MT KENYA