Kazi za ukarabati katika Uwanja wa Kasarani zinaendelea, huku sehemu za muundo wa uwanja huo zikiondolewa ili kutengeneza nafasi kwa ajili ya vyumba sita vipya vya hadhi ya juu (skyboxes), wakati juhudi za kukidhi makataa ya CAF ya tarehe 31 Disemba zikiendelea. Awali, CAF ilitaka Kenya iweke vyumba 61 vya aina hiyo uwanjani hapo, lakini serikali ilitoa hoja kwamba hatua hiyo ingehitaji kubomolewa kwa sehemu kubwa ya uwanja huo kwa muda mfupi kabla ya mashindano ya AFCON ya mwaka 2027. Mashindano hayo ya 'Pamoja' yataandaliwa kwa pamoja na Kenya, Uganda na Tanzania.
Jua linashuhudiwa Makindu, Mtito andei na Voi.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.