Serikali kuu imetenga shilingi bilioni 18 kwa ajili ya ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilomita 270 katika Kaunti ya Elgeyo-Marakwet. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa barabara ya Kipkundul–Kapyego–Kamelei inayounganisha kaunti za Elgeyo-Marakwet na West Pokot, Rais William Ruto alisema serikali yake imedhamiria kuhakikisha hakuna eneo linalosalia nyuma katika maendeleo ya miundombinu. Aliongeza kuwa shilingi bilioni 1.6 zimetengwa kwa ajili ya kuunganisha umeme katika nyumba za kaunti hiyo.


WILLIAM RUTO –CONSTRUCT