Serikali imehimizwa kukusanya Takwimu kuhusu ndoa za utotoni zinazowahusisha wasichana wenye umri wa miaka tisa hadi kumi na miwili, ikiwa ni pamoja na visa ambavyo havijaripotiwa. Mwanzilishi wa Samburu Girls Foundation Josephine Kulea anasema data ya sasa inalenga zaidi wasichana wenye umri wa miaka 14 na zaidi, ikiwaacha waathiriwa wadogo, wengine wenye umri wa miaka minane. Anasema data kamili inahitajika ili kuongoza sera na kuimarisha juhudi za kukomesha ndoa za utotoni.

JOSEPHINE KULEA - LAW