Wanafunzi wa vyuo vikuu watalazimika kusubiri kwa muda mrefu zaidi kabla ya kuanza tena masomo baada ya mazungumzo muhimu kati ya serikali na vyama vya wahadhiri jana kushindwa kufikia makubaliano ya kukomesha mgomo unaoendelea. Maafisa wa UASU na KUSU walikataa ofa ya Sh bilioni 12 kutoka kwa serikali ili warudi kazini. Katibu Mkuu wa UASU Constantine Wasonga alisema kwamba ofa hiyo haitoshi, akisisitiza kwamba serikali inapaswa kutekeleza kikamilifu CBA yao.
CONSTANTINE WASONGA - FIGURES