Mchungaji mwenye umri wa miaka 18 alijeruhiwa katika makabiliano ya risasi yaliyodumu kwa saa nne kati ya wachungaji na watu wanaoshukiwa kuwa majambazi wenye silaha katika eneo la Dakaiye, Loiyangalani, Kaunti ya Marsabit. Tukio hilo lilitokea jumapili baada ya kundi la wachungaji kwenda kutafuta ngamia watatu waliokuwa wamepotea siku iliyotangulia. Kulingana na polisi, wachungaji hao walikuwa wamefanikiwa kupata ngamia sita kati ya tisa waliopotea, walipovamiwa ghafla na idadi ya watu isiyojulikana—wanaoshukiwa kuwa majambazi wenye silaha.