Kiongozi wa Chama cha Jubilee, Fred Matiang’i, na kiongozi wa People’s Party, Ndindi Nyoro, leo watatembelea Kaunti ya Kajiado ili kupigia debe vyama na ajenda zao kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027. Akizungumza awali, Matiang’i alisema kuwa timu hiyo itahutubia wakaazi katika Soko la Oloitoktok kuanzia saa sita mchana kabla ya kuelekea Soko la Kimana saa nane mchana.
FRED MATIANG’I-CAMPAIGN