Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Taifa la Kudhibiti UKIMWI, Nduku Kilonzo, anatoa wito wa kufanyiwa tathmini kwa mageuzi ya kimataifa kuhusu HIV ili kubaini iwapo yanaimarisha juhudi za kinga na utoaji wa huduma katika ngazi ya nchi. Kilonzo, anasema kuwa kuimarisha ufanisi katika ngazi ya kimataifa hakumaanishi moja kwa moja kupatikana kwa matokeo bora zaidi kwa nchi na jamii. Anasema mageuzi hayo lazima yaimarishe uwezo wa serikali katika kukusanya rasilimali na kutoa huduma za kinga dhidi ya HIV pale zinapohitajika zaidi.


NDUKU KILONZO – REFORMS