Mtaalamu wa masuala ya usalama, George Musamali, ameeleza wasiwasi wake kuhusu usalama wa wanafunzi wa vyuo vikuu na vyuo wanaoishi nje ya taasisi hizo, akitaja sababu kama vile kutodhibitiwa kwa mienendo yao na ukosefu wa usalama wa kutosha katika nyumba wanazopangisha. Musamali anasema wanafunzi wengi wanaishi katika mazingira ambayo ni vigumu kufuatilia mienendo na mahali walipo, jambo linalowaweka katika hatari. Kauli yake inafuatia kifo cha Ivy Anyango, mwenye umri wa miaka 22, ambaye mwili wake ulioopolewa katika shimo la maji taka baada ya kutoweka mwezi Juni.


GEORGE MUSAMALI – UNIVERSITIES