Kenya inaboresha sekta yake ya kilimo kupitia maabara za upimaji wa udongo kwa njia ya kidijitali na upimaji mashinani. Akihutubia jukwaa la kimataifa kuhusu maji huko Roma, Waziri wa Kilimo Mutahi Kagwe alibaini kuwa chini ya mpango huu, kila mkulima atapokea pasipoti ya udongo kwa njia ya kidijitali ili kupata pembejeo zilizofadhiliwa na huduma za ushauri zinazoendeshwa na AI. Mkakati huo unalenga kuongeza mavuno ya kilimo kwa kila kitengo, kupunguza bili za uagizaji bidhaa kutoka nje na kuimarisha usalama wa chakula nchini kote.
MUTAHI KAGWE - DIGITAL