Tume ya EACC imemkamata mwalimu wa kike kutoka shule ya upili katika Kaunti ya Bungoma kufuatia madai ya kuitisha Shilingi elfu 300 kutoka kwa walimu watatu wasio na ajira ili kuwasaidia kupata kazi katika TSC. Tume hiyo ilisema kuwa mshukiwa anadaiwa kuitisha Shilingi elfu 100 kutoka kwa kila mmoja wa watafutaji hao wa kazi. Mwalimu huyo alikamatwa jana kufuatia uchunguzi wa awali kuhusu malalamiko kwamba alidai kuwa na uhusiano au watu wa kumsaidia kufanikisha mchakato wa kuajiriwa kwao.