Serikali itafanya ukaguzi upya kwa watengenezaji wote wa pombe katika juhudi zake za kuimarisha vita dhidi ya pombe haramu na bandia kote nchini. Naibu Rais Kithure Kindiki alisema kuwa hata watengenezaji walio na leseni halali watafanyiwa uchunguzi upya ili kubaini iwapo bidhaa zao zinakidhi viwango vinavyohitajika vya afya na ubora. Aliongeza kuwa biashara za watengenezaji watakaobainika kuzalisha pombe hatari kwa wateja zitafungwa.

KITHURE KINDIKI - CHUMA