Rose Mbithe na wanawe wawili watabaki rumande baada ya mahakama kuweka tarehe 4 mwezi ujao kwa ajili ya kupanga tarehe ya uamuzi wao wa dhamana. Daktari wa magonjwa ya akili David Ndetei amepinga kuachiliwa kwao kwa dhamana akidai kwamba mkewe wa zamani Mbithe alikuwa ametishia kumnyang'anya kila kitu na kumwacha chokoraa. Mbithe na watoto wake wanashtakiwa kwa mauaji ya mtafiti wa afya ya akili Victoria Mutiso.

DAVID NDETEI – COURT