Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang'ula ameiagiza Kamati ya Elimu kushughulikia wasiwasi kuhusu usimamizi wa Shule za JSS zilizo ndani ya majengo ya shule za msingi. Wetang'ula ameibua hofu kwamba shule za msingi hazina wafanyakazi wa kutosha na uwezo wa kusimamia rasilimali za umma, akionya kwamba fedha za masomo zinazotumwa kwa taasisi hizo zinaweza kuporwa. Anamtaka mwenyekiti wa kamati Julius Melly kufanya kazi na Wizara ya Elimu ili kuhakikisha wafanyakazi waliohitimu wanasimamia kazi muhimu za JSS.

MOSES WETANG’ULA – JSS