Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro ameendelea kutoa wito wa kufichuliwa kwa wanahisa wa Kiwanda cha Kusafisha mafuta cha Dangote East Africa huko Lamu, na kuibua maswali kuhusu umiliki wa mradi huo wa Sh trilioni 2. Nyoro alisema Wakenya wanastahili kuwajua watu binafsi na mashirika yanayomiliki hisa katika kampuni ya Kenya iliyo nyuma ya kiwanda hicho. Ombi lake linakuja kufuatia uchunguzi kuhusu muundo wa umiliki wa mradi huo, mipango ya ardhi na ahadi za kifedha za Kenya.
NDINDI NYORO - BIDHAA